TUNISIA

Tunisia yaadhimisha miaka 10 tangu maandamano ya umma

Maandamano ya umma nchini Tunisia mwaka 2011
Maandamano ya umma nchini Tunisia mwaka 2011 Alessandro Bajec

Tunisia inaadhimisha miaka 10 tangu kufanyika kwa maandamano makubwa ya wananchi yaliyomwondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Zine El Abidine Ben Ali.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo ambayo yalichochea kuanza kushuhudiwa harakati za kutaka mageuzi katika nchi za kiarabu, zilisababisha kiongozi huyo wa Tunisia kuikimbia nchi yake.

Miaka iliyopita, siku kama ya leo, kulikuwa na maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo lakini, mwaka huu hali hiyo haijashuhudiwa kutokana na masharti ya watu kutotembea nje kutokana na janga la corona.

Maaandamano hayo yalianza baada ya mchuuzi Mohamed Bouazizi kujiua kutokana na ugumu wa maisha, hatua ambayo ilisababisha safari ya nchi hiyo kutaka serikali mpya, katiba mpya na kushinikiza maisha yao kubadilika.

Wakati wananchi wa taifa hilo wanapokumbuka siku hii, mashirika ya kutetetea haki za kibinadamu yataka mamlaka nchini humo kuwafidia watu waliojeruhiwa au haki zao kukiukwa wakati wa maandamano hayo.