ETHIOPIA

Waziri wa zamani wa mashauriano ya kigeni wa Ethiopia auawa na Jeshi

Jeshi la Ethiopia
Jeshi la Ethiopia Reuters

Vikosi vya jeshi la Ethiopia vimetangaza kumuua waziri wa zamani wa mashauriano ya kigeni wa Ethiopia Seyoum Mesfin, mmoja wa wanachama waanzilishi wa chama Tigray People’s Liberation Front (TPLF) ambaye wanamtuhumu kuansisha uasi na serikali ya Ethiopia kwa lengo la kutaka jimbo la Tigray kujitenga.

Matangazo ya kibiashara

Katika yake yake, jeshi limesema kuwa Bw.Seyum, aliuawa pamoja na wanachama wengine wa ngazi ya juu wa chama cha TPLF kaskazini mwa jimbo la Tigray, baada ya kupinga wito wa kujisalimisha.

Seyoum Mesfin alihudumu kama waziri wa mashauriano ya kigeni kutoka mwaka 1991 hadi 2010. Serikali ilikuwa ikimsaka- pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu katika chama cha TPLF.

Awali serikali ya Ethiopia ilitangaza zawadi ya birr milioni 10 sawa na dola 254,000 kwa yoyote atakayetoa taarifa zitakazosidia kukamatwa kwao.