DRC

Mkaguzi mkuu wa jeshi, luteni jenerali Tim Mukunto aaga dunia

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwa Mashariki mwa nchi hiyo
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwa Mashariki mwa nchi hiyo REUTERS/Goran Tomasevic

Mkaguzi mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, FARDC, amefariki dunia leo Ijumaa nchini Afrika Kusini. Kulingana na chanzo kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka wa jeshi, Luteni Jenerali Tim Mukunto alikuwa ameambukizwa virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Mukunto aliteuliwa kuwa mkaguzi mkuu wa jeshi mnamo mwaka 2018, kabla ya kuteuliwa tena mnamo mwezi Februari 2020 na rais Felix-Antoine Tshisekedi.

Tangu aingie madarakani, Jenerali Mukunto alishughulikia kibinafsi mashtaka katika kesi ya watu wanaodaiwa kuwa wauaji wa wataalam wa Umoja wa Mataifa huko Kasai. Alizuru mara kadhaa mji wa Kananga, ambapo aliwakilisha upande wa mashtaka katika vikao vingi kuhusiana na kesi hiyo.

Wakati wa mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Okapi, mnamo mwaka 2019, Jenerali Tim Mukunto aliahidi familia za Zaida Catalan na Michael Sharp 'ataweka sawa kinachowezekana kupitia njia zote za kibinadamu na kiufundi ili ukweli ujulikane kuhusu mauaji ya wataalam'.