DRC

Tshisekedi akutana na Katumbi na Bemba kuhusu muungano mpya

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini DRC katika kikao kilichopita
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini DRC katika kikao kilichopita twitter.com/moise_katumbi

Suala la uundwaji wa muungano wa kisiasa utakao wezesha maendeleo katika siasa ya DRC bado unaendelea kuibua maswali mengi nchini humo, licha ya jitihada kutoka upande wa rais Félix-Antoine Tshisekedi.

Matangazo ya kibiashara

Rais Félix-Antoine Tshisekedi na washirika wake wakuu Jean-Pierre Bemba wa chama cha MLC na Moïse Katumbi kutoka muungano wa Ensemble pour la République, akiwemo kiongozi wa mpito wa chama cha UDPS Jean-Marc Kabund.

Kama wakati wa mkutano wao uliopita wa Desemba 26, Jean-Pierre Bemba na Moïse Katumbi walisisitiza kujua lengo la umoja mtakatifu wa kitaifa.

Kulingana na vyanzo vyetu, wawili hao walisisitiza juu ya hoja ya kuujumuisha muungano huo katika mahitaji ya kila siku na maswala ya Wakongo.

Kama kuendelea kwa ukosefu wa usalama na mauaji huko Mashariki mwa DRC, ukiukaji wa uhuru wa nchi, uchumi, au mfumo wa elimu ya bure ambao utekelezaji wake ni mbovu.

Katika orodha hii, kuna haki za kimsingi ambazo haziheshimishwi: afya, utoaji wa msaada wa chakula, upatikanaji wa maji safi na umeme ... "Ni muhimu kuweka na kuzingatia vipaumbele vya utawala kwa kuwaangalia mahitaji ya wananchi, ”anasema Chérubin Okende, naibu kiongozi wa kitaifa wa vuguvugu la Moïse Katumbi.

Kujiunga kwa wajumbe wa muungano wa FCC katika mchakato huo kunawatia wasiwasi viongozi hao wawili wa Lamuka, hasa uwezekano wa kuona wafuasi wa zamani wa Joseph Kabila wakijadili kuhusu nafasi ya uongozi wa ofisi kuu ya Bunge la taifa.