JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Umoja wa Mataifa wasema raia wa Jamhuri ya Kati wanakimbilia nchini DRC na Cameroon

Moja ya barabara ya Bangui
Moja ya barabara ya Bangui RFI / Gaël Grilhot

Idadi ya watu wanaokimbia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na utovu wa usalama, imeongezeka wiki hii na kufikia Elfu Sitini.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu zaidi ya Elfu Hamsini wamekimbia nchi hiyo wakipitia mto Ubangui nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Siku ya Jumatano wiki hii; watu wengine Elfu 10 pia waliwasili nchini DRC wakitokea katika jiji kuu la Bangui.

Wiki hii, kulishuhudiwa makabiliano kati ya waasi na wanajesshi wa serikali, waliotaka kuteka jiji kuu Bangui suala ambalo limeongeza idadi ya watu wanaokimbia nchi hiyo kuongezeka.

Mbali na DRC wakimbizi wengine wamekimbilia nchini Cameroon huku wengine wakisalia nchini humo.

Nchi hiyo imeendelea kushuhudia wasiwasi wa kuzuka kwa mapigano baada ya waasi kuungana na kutaka kutofanyika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Desemba mwaka uliuopita.