AFRIKA

COVID-19: Umoja wa Afrika wapata chanjo milioni 270 kwa bara hilo

Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani.
Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani. REUTERS

Umoja wa Afrika umepata dozi milioni 270 za chanjo za kupambana dhidi ya COVID-19 ambazo zitasafirishwa kwa nchi za bara hilo.

Matangazo ya kibiashara

Dozi milioni 50 zitapatikana kati ya mwezi Aprili na Juni. Dawa hizo zitakazotumiwa kwa chanjo zimenuliwa na Umoja aw Afrika kutoka maabara ya Pfizer, AstraZeneca na Johnson & Johnson.

Chanjo hiyo sio dawa pekee kwa Afrika kukabiliana na COVID-19. Afrika pia itanufaika na mfumo wa Covax uliozinduliwa na shirika la Afya Duniani (WHO), na  hatua zilizochukuliwa katika mataifa mbalimbali ya bara la Afrika.

Hii ni ishara kubwa kutoka kwa Umoja wa Afrika. Chanjo milioni 270 zitanunuliwa kutoka maabara ya Pfizer na AstratZeneca, kati ya mengine.

Lakini Afrika haijakata tamaa juu ya mpango wa Covax, uliozinduliwa na shirika la Afya Dunia na nchi tajiri, ili kuweka kiwango sawa cha huduma kwa nchi zote kwa chanjo zilizotengenezwa ulimwenguni.

Umoja wa Afrika tu unaogopa kwamba kiwango kilichotolewa na COVAX kwa kipindi kati ya mwezi Februari na Juni hakitatosha kuwapa chanjo wafanyakazi wa afya.