MALAWI

Shule zafungwa nchini Malawi kwa wiki tatu

Kirusi cha corona
Kirusi cha corona NEXU Science Communication | Reuters

Serikali ya Malawi imechukua uamuzi wa kufunga shule zote nchini humo kwa wiki tatu kuanzia leo, ili kudhibiti ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona Corona.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa taifa, rais Lazarus Chakwera ametangaza masharti ya watu kutotembea kati ya saa tatu usiku mpaka Alfajiri.

Tangu kuanza kwa mwezi huu wa Januari, watu 300 wameambukizwa virusi hivyo.

Malawi imerekodi visa 12,470 vya maambukizi baada ya visa vipya 685 kuthibitishwa, na vifo 314, baada ya vifo 14 kuthibitishwa