SUDAN

Watu zaidi ya 50 waangamia katika mapigano ya kikabila Kusini mwa Sudan

Jeshi la UNAMID likiwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan
Jeshi la UNAMID likiwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan Reuters

Mauaji mengine yaliyotokea katika jimbo la Darfur, nchini Sudan yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 50 Kusini mwa sudan, siku chache baada ya zaidi ya watu 80 kuangamia mwishoni mwa wiki iliyopita Magharibi mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya kikabila yamesababisha vifo vy watu zaidi ya 55 na 37 wamejeruhiwa kulingana na vyanzo kutoka nchini humo.

Mapigano hayo ni kati ya kabila kutoka jamii ya Waarabu na wale wasio kiwa Waarabu ya kupigana kati ya makabila ya Kiarabu na

Gavana ametangaza sheria ya kutotoka nje na kupelekwa kwa askari na maafisa wa usalama zaidi kutoka mashariki mwa Darfur.

Eneo la al-Tawil limekuwa eneo la mapigano kati ya kabila la Kiarabu la Rizeigats na kabila lisilo la Kiarabu la Fallata.

Baada ya mauaji yaliyotanguliwa na kulipiza kisasi ambayo tayari ilikuwa imewaua watu kadhaa wiki iliyopita. Jamii hizo mbili hukabiliana mara kwa mara katika mzunguko wa vurugu za kulipiza kisasi kwa miongo kadhaa.

Tayari mwaka jana kulikuwa na mzozo kati ya makundi hayo mawili juu ya wizi wa ng'ombe. Usuluhishi ulisababisha kutiwa saini kwa kusitisha uhasama mnamo
mwezi Mei.