SUDAN

Machafuko Darfur: Idadi ya vifo yaendelea kuongezeka

Raia wa Sudan, wakiîta kando na gari ya walinda amani wa umoja wa Mataifa.
Raia wa Sudan, wakiîta kando na gari ya walinda amani wa umoja wa Mataifa. AFP

Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka baada ya machafuko mwishoni mwa wiki iliyopita magharibi mwa Darfur, nchini Sudan. Kulingana na chama kimoja cha madaktari idadi ya watu waliouawa katika machafuko hayo imeongezeka hadi 159, huku 203 wamejeruhiwa na 90,000 wameyatoroka makazi yao.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yaliibuka baada ya mtu kutoka kabila la Kiarabu kuuawa na mtu asiye Mwarabu. Baada ya tukio hilo, visa vya ulipizaji kisasi vilifuata. Na kama vurugu zimetulia, hali inaendelea kuwa ya wasiwasi.

 

Kulingana na mashahidi kadhaa, wanamgambo bado wako ndani ya kambi ya wakimbizi ya Krinding, eneo kuu lililolengwa na mashambulizi hayo.

 

Video zinazosambaa, zinaonyesha nyumba zilizochomwa na kuteketea kwa moto hadi kuwa majivu. Vyanzo kadhaa vinadai kuwa bado kuna miili ndani ya nyumba hizo, ikiongeza hofu ya kuongezeka kwa idadi ya watu waliouawa.

 

Wakimbizi wa ndani walio kuwa wakiishi katika kambi hiyo wamekimbilia eneo jirani. Zaidi ya nusu inasemekana wako katika mji wa El Geneina, wamepewa hifadhi katika shuleni na majengo ya serikali, wengine wamepata hifadhi katika vijiji jirani.