SENEGAL

Senegal yakabiliwa na mlipuko wa pili wa COVID-19, wahudumu wa afya washinikizwa

Picha ikionesha pwani ya nchi ya Senegal
Picha ikionesha pwani ya nchi ya Senegal AP Photo/Javier Fergo

Chama cha madaktari wa dharura kinaonya juu ya ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo, na kubaini kwamba virusi "vinaenea kwa kasi katika mikoa ya Dakar, Thiès, Diourbel, Saint Louis na Kaolack".

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limetoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya na raia kuwa makini zaidi katika kuheshimu hatua za kukabiliana na ugonjwa huo hatari, na kubaini kwamba bado idadi ya wauguzi waliotumwa katika vituo vya matibabu bado ni ndogo.

Utangazaji

 

Tangu kuzuka kwa virusi hivyo kwa mara ya kwanza nchini Senegal, Dk Khady Fall, mtaalam wa ganzi katika hospitali ya Dalal Jamm huko Guédiawaye, amekiri kuwa amechoka kwa kazi anayoifanya kukabiliana na virusi vya Corona.

 

“Tumechoka kwelikweli. Tulianza kazi hii mwezi Machi na hadi sasa hatupumzika kabisa. Lakini ni lazima tupambane, dhidi ya janga hili baya, " Dk Khady Fallamesema.

 

Katika mkoa wa Matam, kaskazini mashariki mwa Senegal, kituo cha matibabu cha Ourossogui (CTE) hupokea wagonjwa walio katika hali mahututi kituo hiki kina vitanda vitano vya wagonjwa mahututi. Huduma ambayo inakabiliwa na shinikizo kubwa. "Ni kazi ngumu sana, hasa kwa idadi hii ya wafanyikazi ambao ni wachache," Dkt Ndiaye Diop, mmoja wa maafisa wa afya amesema.

 

"Wafanyakazi huzunguka katika wodi za hospitali. Leo katika wodi ya wagonjwa mahututi, kesho katika CTE" kwa sababu "sio tu COVID, kunamagonjwa mbalimbali hapa, na watu wanakuja katika hali mahututi, na magonjwa yote haya tunapaswa kukabiliana nayo, " ameongeza.

 

Kulingana na Wizara ya Afya, Senegal hadi sasa imerekodi vifo 546 vinavyotokana na ugonjwa huo.