MSUMBIJI

Kimbunga Eloise chasababisha uharibifu mkubwa Beira

Hasara iliyojitokeza baada ya kimbunga katika mji wa Beira
Hasara iliyojitokeza baada ya kimbunga katika mji wa Beira RFI/Cristiana Soares

Mji wa Beira na viunga vyake umekumbwa na mafuriko kutokana na kumbunga Eloise, wakaaei wengi kutoka maeneo hayo wamelazimika kuyahama makaazi yao, na majumba kadhaa yameporomoka, huku mashamba yakisomwa na maji kutokana na mafuriko hayo.

Matangazo ya kibiashara

Maeneo mengi ya Msumbiji ya kati yapo chini ya maji. Mengi kati ya maeneo hayo ni yale ya mashambani ambapo kuna hofu kwamba watu wengi watapoteza mazao yao .

Kulingana na Taasisi ya kitaifa ya hali ya hewa nchuni humo INAM, mji wa Beira umeingiliwa maji yenye ujazo wa milimita 250 kutokana na mvua zilizonyesha katika kipindi cha saa 24.

Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka mji huo, serikali inajaribu kurudisha umeme na mawasiliano ambayo yalikatwa katika baadhi ya maeneo, na watu kadhaa wameuawa.

Zaidi ya nyumba 1,000 zimeangamizwa na nyengine 3,000 zikiharibiwa vibaya, kulingana na maafisa wa Taasisi ya usimamizi wa majanga.

Kimbunga hiki kimetabiriwa kuelekea Zimbabwe na kaskazini mwa Afrika Kusini mataifa ambayo tayari yamekumbwa na mvua kubwa.