TUNISIA

Tunisia: Wanajeshi 4 wauawa katika mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini

Polisi wa nchini Tunisia.
Polisi wa nchini Tunisia. Hatem SALHI / AFP

Wanajeshi wanne wa Tunisia waliuawa Jumatano wiki hii katika mlipuko wa bomu la akutegwa ardhini katika eneo lenye milima katikati mwa Tunisia wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi, msemaji wa Wizara ya Ulinzi Mohamed Zekri ameliambia shirikja la habari la AFP. 

Matangazo ya kibiashara

"Wanajeshi wanne ambao walikuwa sehemu ya kitengo cha jeshi kilichohusika na kufanya operesheni katika Mlima Mghila kutafuta magaidi, waliuawa katika mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji," amesema.

Ujumbe huu "uko ndani ya mfumo wa operesheni za kukabiliana na ugaidi unaofanywa mara kwa mara na vikosi vya jeshi katika jimbo hili," Zekri ameongeza.

Mlima Mghila ambao unapatikana katika sehemu ya milima mirefu inayopakana na Algeria, unachukuliwa kama ngome kuu ya maficho ya wanamgambo wa kijihadi katika eneo hili.

Jeshi limekuwa liyatimuwa makundi yenye silaha katika eneo hilo tangu mwaka 2012. Kundi la Okba Ibn Nafaa phalanx, lenye mafungamano na Al-Qaeda, ni moja ya makundi yanayopiga kambi katika eneo hilo lenye milima.

Kundi hili liliwahi kufanya shambulio mwaka 2014 kwenye Mlima Chaambi, shambulio baya zaidi dhidi ya jeshi (askari 15 waliuawa) na wakati huo ndipo kulianza mashambulio mabaya nchini Tunisia.

Baada ya mapinduzi ya mwaka 2011, Tunisia ilikabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi ya kijihadi, hasa katika mkoa wa mpaka wa Algeria na Libya.

Hali ya usalama imeimarika sana katika miaka ya hivi karibuni, lakini mashambulio ya mara kwa mara yanaendelea kulenga vikosi vya usalama.