WTO

WTO: Marekani yamuunga mkono mgombea wa Nigeria Okonjo-Iweala

Ngozi Okonjo-Iweala, anayetarajiwa kuwa mkurugenzi wa WTO
Ngozi Okonjo-Iweala, anayetarajiwa kuwa mkurugenzi wa WTO AFP Photos/Fafbrice Coffrini

Marekani imesema inamuunga mkono Ngozi Okonjo-Iweala, raia wa Nigeria kwenye nafasi ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) baada ya mpinzani wake wa Korea Kusini kujitoa.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili lilitolewa na ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani kwa niaba ya utawala wa Rais Joe Biden.

Ngozi Okonjo-Iweala, 66, hapo awali kuwania kwake kwenye nafasi hiyo kulikuwa kumekabiliwa na upinzani kutoka kwa rais wa zamani DonaldTrump.

Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara katika utawala wa Donald Trump ilitoa taarifa ikimuunga mkono rasmi mgombea mwingine pekee aliyebaki, waziri wa biashara wa Korea Kusini Bibi Yoo Myung-hee, ikimsifu kwa kuwa mpatanishi wa mazungumzo yenye mafanikio ya biashara na ujuzi

anaohitaji kuongoza shirika hilo la biashara katika "wakati huu mgumu sana."

Okonjo-Iweala, waziri wa zamani wa fedha na mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Dunia, atakabiliwa na changamoto kubwa huku madola pinzani yakilumbana wakati kukiwa na ongezeko la mivutano na ulinzi wa masoko wakati wa mporomoko wa kibiashara unaosababishwa na janga la virusi vya corona.