CHAD

Wapinzani kadhaa wa Chad washikiliwa na idara ya usalama

Rais wa Chad, Idris Deby
Rais wa Chad, Idris Deby wotzup.ng

Wanasiasa kadhaa wa upinzani dhidi ya rais wa Chad Idriss Déby Itno, ambaye yuko madarakani kwa miaka 30, wanazuiliwa jela tangu Jumatatu wiki hii na watahukumiwa kwa kukaidi marufuku ya maandamano siku ambayo rais wa nchi hiyo alitangazwa kuwania katika uchaguzi wa urais kwa muhula wa sita, waziri mmoja amesema.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi, wakati chama cha Bwana Déby, 68, ambaye anaongoza Chad kwa mkono wa chuma tangu mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1990, alipoteuliwa kupeperusha bendera ya chama tawala katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Aprili 11 mgombea urais mnamo Aprili 11, wanasiasa wa upinzani waliandama katika mi wa N'Djamena kudai " kuwepo na mabadiliko katika utawala "na" haki ya kijamii "izingatiwe.

Lakini mikutano ya hadhara, kwa wito wa vyama vya upinzani ambao walikuwa na nia ya kuandamana "kwa amani", ilipigwa marufuku na polisi walitumia nguvu za kupita kiasi kujaribu kuzima maandamano hayo Jumamosi wiki iliyopita.

Watu kadhaa walikamatwa, ikiwa ni pamoja na Mahamat Nour Ahmed Ibedou, katibu mkuu muungano wa mashirika yanayotetea haki za binadamu (CTDDH), na mkosoaji mkubwa wa serikali.