G5 SAHEL

Ufaransa kuendelea kuwepo kijeshi katika miezi ijayo katika Ukanda wa Sahel

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Thibault Camus/Pool via REUTERS

Rais wa Ufaransa ametoa wito wa kuyatokomeza makundi ya kijihadi yenye mafungamano na al-Qaeda katika ukanda wa Sahel.

Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron amezungumza baada ya kushiriki kwa njia ya video mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa G5 Sahel unaofanyika katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena.

Hafla hiyo ilikuwa fursa ya kuangalia hatua zilizotekelezwa tangu mkutano wa Pau, mwaka mmoja uliopita, nchini Ufaransa. Na rais wa Ufaransa pia ametangaza kuwa hakutakuwa na suala la kupunguza wanajeshi wa kikosi cha Ufaransa cha Barkhane katika miezi ijayo.

"Katika miezi ijayo uwepo wetu wa kijeshi katika ukanda wa Sahel hautabadilika na tutazindua operesheni zingine kubwa," amesema Emmanuel Macron. Kikosi cha Barkhane kwa hivyo kitabaki kikiwa na zaidi ya wanajeshi 5,000, na suala la wanajeshi 600 wa ziada kusaidi kikosi cha Barkhane, uamuzi uliochukuliwa mwaka mmoja uliopita huko Pau bado halijabadilika.

Katika wiki za hivi karibuni, kufuatia mafanikio ya kijeshi yaliyopatikana dhidi ya kundi la Islamic State katika eneo la Grand Sahara, Ikulu ya Élysée ilifikiria kupunguza idadi ya wanajeshi wake.

Lakini rais Macron ameelezea juhudi za kijeshi zilizopelekea ushindi na ameruhusu kuokoa ukanda wa Sahel mara ya pili, huku akibaini kuwaondoa kikosi chetu cha Barkhane katika eneo hili itakuwa kosa kubwa.