Milio ya risasi yasikika wakati wa maandamano ya upinzani nchini Somalia
Imechapishwa: Imehaririwa:
Milio ya risasi ilisikika wakati wanasiasa wa upinzani nchini Somalia walipojairbu kuandamana jijini Mogadishu, kuishtumu serikali kwa kushindwa kuandaa Uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka uliopita na baadaye kuahrishwa hadi mwezi Februari.
Umoja wa Mataifa na ule wa Afrika, umemshtumu kutokea kwa makabiliano hayo na kutaka pande zote kuketi katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu kuhusu mvutano huo wa kisiasa.
Muhula wa rais Mohamed Abdullahi Mohamed, ulimalizika wiki iliyopita, na kuingiza nchi hiyo kwenye mvutano wa kisiasa.
Kabla ya jaribio hilo la maandamano, barabara kadhaa zilifungwa na maafisa wa usalama kushika doria, baada ya kuwepo kwa madai kuwa watu wenye silaha walijaribu kushambulia makaazi ya rais.
Rais Farmajo amekuwa katika mkutano wa siku mbili, siku ya Alhamisi na Ijumaa, kujadili mustakabali wa kisiasa wa nchi hiyo.