SUDAN- SIASA

Raia wa Sudan kuanza kupata malipo ya posho za kila mwezi

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, february 8 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo, february 8 2017. REUTERS/Feisal Omar

Fedha za wafadhili kwa ajili ya mpango unaolenga kulipa posho za kila mwezi za dola 5 kwa raia wengi wa nchi ya Sudan zitatolewa kwa wizara ya fedha kuanzia leo Jumatatu baada ya nchi hiyo kuridhia kupunguza thamani ya sarafu yake, Gavana wa benki Kuu ya Sudan amesema.

Matangazo ya kibiashara

Kupunguzwa kwa thamani ya paundi ya Sudan ni moja ya mageuzi magumu yaliyopendekezwa na shirika la fedha la kimataifa IMF ili kuisaidia nchi hiyo kupata nafuu ya kulipa deni lake na kuvutia wawekezaji.

Kutolewa kwa dola milioni 400 kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mpango huo kulicheleweshwa kutokana na wasiwasi kuwa thamani kamili ya posho hizo ingepungua kabisa chini ya kiwango cha ubadilishanaji wa sarafu ambacho hakijafanyiwa mageuzi.

Mamlaka nchini Sudan imetolewa wito raia kuwa na uvumilivu wa mageuzi ya kisera yanayofanyika kwa sasa ikibani kwamba leo lake kuu ni kutetea maslahi ya raia wake.