Kesi ya rushwa dhidi ya Jacob Zuma, kuanza mwezi Mei
Imechapishwa:
Kesi ya rushwa ya dolla billioni 2, dhidi ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na kampuni ya Ufaransa, Thales, itaanza kuskizwa namo mwezi Mei 17, mahakama ya kikatiba nchini humo imesema.
Zuma anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kipindi alihudumu kama makamo rais mwaka 1999-2009, na rais kutoka mwaka 2009- 2018, japo amekanusha taarifa hizo.
Zuma anakabiliwa na mashtaka 16 ya udanganyifu, rushwa na utakatishaji wa fedha akishirikiana na kampuni ya silaha ya Ufaransa ya Thales.
Zuma anatuhumiwa kupokea hongo ya dolla 34,000, kila mwaka, kuanzia mwaka 1999 kutoka kwa kampuni ya Thales, ikiwa njia ya kuikinga kampuni hiyo kutochunguzwa kwa kashfa tata ya kuuzia salaha jeshi la Afrika kusini.
Thales kwa upande wake kadhalika imekanusha kuhusika kutoa pesa zozote kwa Zuma kama hongo.