LIBYA-USALAMA-SIASA

Libya: mvutano kati ya wanamgambo wazuia mchakato wa amani

Waziri wa mambo ya Ndani wa Libya, Fathi Bachagha, aliyenusurika kifo.
Waziri wa mambo ya Ndani wa Libya, Fathi Bachagha, aliyenusurika kifo. Mahmud TURKIA AFP

Nchini Libya, wanasiasa wamegawanyika juu ya mazingira ya kile kilichotokea Jumapili Februari 21 kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Fathi Bachagha, kiongozi mwenye ushawishi kutoka Magharibi mwa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Ndani anasema lilikuwa "jaribio la kumuua lililoandaliwa vizuri na sio bahati mbaya" wakati maafisa kadhaa huko Tripoli wanasema ni mizozo kati ya wanamgambo wanaokinzana ambayo husababisha machafuko.

 

Jaribio la madai ya kumuua waziri huyo linaongeza hofu ya kuanza tena kwa vurugu katikati ya juhudi za mpito za kisiasa.

Nchini Libya, kuna zaidi ya silaha milioni 29 zinazomilikiwa na raia kinyume cha sheria, na nchi hiyo pia inakumbwa na ubabe wa wanamgambo na mapambano ya ushawishi. Aina hii ya tukio hufanyika mara kwa mara. Vitisho vingine vikali pia vililenga Waziri Mkuu Fayez Sarraj na wanasiasa wengine. Hii inaonyesha jinsi gani hali ya usalama inavyodorora na husababisha ushawishi kati ya makundi ya wanamgambo wenye nguvu Magharibi mwa Libya.

Utawala mpya wa Abdelhamid Dbeiba, aliyechaguliwa  Februari 5, unaangalia kwa makini makundi haya ya wanamgambo. Tukio lililomkumba Waziri wa Mambo ya Ndani linaonyesha hatari ambayo utawala mpya unaweza kukabiliana nayo, hasa ikiwa inajaribu kudhibiti ushawishi wa wanamgambo. Katika muktadha huu, mustakabali wa mchakato wa kisiasa unaweza kuwa hatarini.