ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Raia kutoka la jimbo la Tigray waishi kwa hali ya hofu

Walinda amani wa kikosi cha UNMISS huko Juba, Agosti 31, 2016 (picha ya kumbukumbu).
Walinda amani wa kikosi cha UNMISS huko Juba, Agosti 31, 2016 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Jok Solomun

Angalau walinda amani 15 wa Ethiopia kutoka operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa huko Sudani Kusini, UNMISS, waliomba hifadhi ya ukimbizi Jumatatu (Februari 22) huko Juba walipokuwa karibu kuanza safari ya kurudi Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Walinda amani hao 15 kutoka UNMISS, wote ni kutoka mkoa wa Tigray, ambapo mamlaka ya shirikisho inafanya operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la waasi la TPLF.

Tangu kuanza kwa mzozo huo, maafisa na askari kutoka jimbo la Tigray wanaishi katika hali ya hofu.

Tukio la Jumatatu katika uwanja wa ndege wa Juba sio la kwanza kuonyesha kuwa raia kutoka jimbo la Tigray nchini Ethiopia sasa wanaishi chini ya shinikizo.

Walinda amani ambao walikataa kwenda Addis Ababa waliwaambia abiria wa Sudan Kusini ambao waliwasaidia kwamba wanahofia maisha yao ikiwa watarudi nchini.