ETHIOPIA - USALAMA - TIGRAY - GIJET

Mamia ya nyumba ziliteketezwa jimboni Tigray, utafiti umebaini

Baadhi ya nyumba zilizoteketezwa jimbino Tigray, nchini Ethiopia.
Baadhi ya nyumba zilizoteketezwa jimbino Tigray, nchini Ethiopia. EDUARDO SOTERAS AFP

Zaidi ya nyumba 500, ziliteketezwa kimakusudi katika mji wa Gijet, jimboni Tigray nchini Ethiopia, haya ni kwa mjibu wa Utafiti wa shirika la satellite imagery, utafiti unaoashiria kuwa bado kuna mzozo unaoendelea jimboni Tigray.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu Abiy Ahmed, alitangaza mwezi novemba mwaka uliopita, kuwa wanajeshi wake walifanikiwa kudhibiti wanajeshi wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF), waliokuwa watiifu wa serikali ya Tigray.

Hata hivyo, imebainika kuwa bado kuna vita vinavyoendelea kwa baadhi ya sehemu za jimbo hilo, kwa mjibu wa wenyeji na umoja wa Mataifa.

Serikali ya Ethiopia imekiri kuwepo kwa visa vichache ya ufyatulianaji wa risasi jimbo Tigray, ila imesema hali ya usalama jimboni humo imedhibitiwa.

Kaimu kiongozi wa serikali, jimboni Tigray, Mulu Nega, amesema ametuma kamati maalamu kuchunguza hali katika mji wa Gijet.

Katika ripoti ya shirika la utafiti wa mikasa la DX Open Network, lenye makao yake nchini Uingereza imesema kwa mjibu wa picha ilizodadisi za moto katika mji wa Gijet, moto huo haukuwa ajali.

DX Open Network hata hivyo katika ripoti yake haijaeleza ni nani waliohusika katika mkasa huo wa moto.

Serikali ya Ethiopia na ile ya Tigray, zote zimekataa kuhusishwa na mzozo wa jimbo la Tigray, wakati huu tatizo la mawasiliano katika jimbo la Tigray zikisalia kuwa kitandawili, kwani serikali bado inadhibiti mawasiliano jimboni humo.