NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Watu 36 wauawa katika mashambulio mawili Nigeria

Jeshi la Nigeria laendelea kukabiliana na makundi ya watu wenye silaha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Jeshi la Nigeria laendelea kukabiliana na makundi ya watu wenye silaha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Audu Marte AFP

Watu wenye silaha wasiojulikana wamewaua watu 36 katika mashambulio mawili ya hivi punde Kaskazini mwa Nigeria, kulingana na maafisa na  ndugu wa wahanga.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yamefanyika katika muda wa saa 48 zilizopita katika majimbo ya Kaduna na Katsina na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Washambuliaji walichoma moto nyumba kadhaa, hali ambayo imesababisha watu kuhama makaazi yao.

Wiki iliyopita, watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia shule ya upili katika jimbo la Niger, nchini Nigeria, na kuwateka nyara wanafunzi 27, wafanyakazi na familia zao.