DRC- USALAMA

Watu zaidi ya 10 wauawa kikatili mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi wa FARDC kwenye eneo la Rwangoma, baada ya mauaji mjini Beni, mashariki mwa DRC, usiku wa jumamosi kuamkia Jumapili Agosti 14 2016.
Wanajeshi wa FARDC kwenye eneo la Rwangoma, baada ya mauaji mjini Beni, mashariki mwa DRC, usiku wa jumamosi kuamkia Jumapili Agosti 14 2016. Sonia Rolley / RFI

Watu wasiopungua kumi na watatu wameuawa kikatili, miongoni mwao askari mmoja wa jeshi la serikali, usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano katika mashambulizi mawili yanayodaiwa kuwa yalitekelezwa na waasi wa ADF mashariki mwa DRC. Vyanzo vya kiusalama vimeripoti

Matangazo ya kibiashara

Mauaji haya yanafanyika huku jeshi la nchi hiyo likidai kufanikiwa kuua muasi mmoja  katika mashambulizi 3 tofauti mkowani kivu kaskazini na mkowani Ituri usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano ya 24 februari na mali mingi kuharibiwa  

Mwenyekiti wa sekta ya Rwenzori huko Kivu Kaskazini Bozi Sindiwako anasema huenda idaidi ya watu waliouawa ikaongezeka taarifa ambayo pia imethibitishwa na mkuu wa mji wa Oicha Nicolas Kikuku baada ya kushuhudia mauaji mapya hayo yaliyofanyika.

Wataalam kutoka Shirika linalokadiria masuala ya kiusalama Barometer of security in Kivu (KST) wanasema mbali na mauaji ya Kisima watu wengine wawili waliuawa katika shambulio lingine usiku huo huo huko Oicha.

Kwa upande wake msemaji wa jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika oparesheni zinazolenga kuwatimua waasi hao luteni Antony Mwalushay ni kuwa askari wao walifanikiwa kumuua muasi mmoja na kunyanganya silaha pamoja na mali zilizokuwa zimeporwa na waasi wa ADF kwenye miji ya Oicha na Kisima.

Hili ni shambulizi la tatu kufanyika juma hili baada ya shambulizi lililolenga  mji wa ndalya mkowani Ituri, ambapo kituo cha afya na maduka pamoja na makaazi ya watu vilivyochomwa moto na waasi huku raia wengine kumi waliuawa kikatili katika vijiji vya Musandaba na Mighende wilayani Beni katika tukio la hivi karibuni.

Wakaazi wa maeneo hayo wamemtaka rais Felix Tshisekedi kuingilia kati katika kuimarisha usalama wa wananchi wa eneo hilo.