ETHIOPIA-AMNESTY INTERNATIONAL-USALAMA

Ethiopia: Jeshi la Eritrea lashtumiwa kwa mauaji ya watu wengi Aksum

Mji wa Aksum, Ethiopia.
Mji wa Aksum, Ethiopia. Creative commons/Jialiang Gao

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limetoa ripoti juu ya kile inachoamini kuwa mauaji ya watu wengi katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, linalokabiliwa na vita vya karibu miezi minne.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linasema vita vinaendeshwa pasipokuwa na mtu yeyote ambayo anaweza kutoa habari sahihi kinachojiri katika jimbo hilo, baada ya njia zote za mawasiliano kukatwa na mamlaka nchini Ethiopia.

Kutokana na hali hiyo, Amnesty International inasema ni vigumu kufanya uchunguzi.

Mlipuko huo wa machafuko inasemekana ulitokea katika mji wa Aksum, mji wa tatu kwa ukubwa huko Tigray, mwezi Novemba uliyopita. Mauaji ya watu wengi, adhabu ya pamoja kwa watu wengi, vimeshuhudiwa kulingana na mshauri Jean-Baptiste Gallopin, ambaye alishirikiana na shirika la Amnesty International, akihojiwa na mwandishi wetu huko Addis Ababa, Noé Hochet-Bodin.

Anasema, "ni mauaji yaliyotokea katika muda wa saa 24 Novemba 28 na 29, yaliyotekelezwa na askari wa Eritrea, kwa kukabiliana na shambulio la kundi dogo la wapiganaji kwenye kambi ya wanajeshi wa Eritrea  katika mji wa Aksum. "

Siku kumi zilizopita, RFI iliripoti habari kutoka kwa profesa ambaye aliripoti mauaji na ugaidi ulitekelezwa kwa wiki kadhaa. Ni vigumu kwa wakati huu kujua idadi ya vifo, lakini Amnesty International inakadiria kuwa mamia kadhaa ya watu waliuawa.

Mauaji hayo yalikuwa kilele cha mfululizo wa ukiukaji ambao ulitanguliwa na mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa kiholela na kufuatiwa na mauaji kwa watu waliokuwa mikononi mwa vyombo vya dola. Katika kipindi hiki, vikosi vya Eritrea pia vilipora katika maduka na makampuni mblimbali ya mji wa Aksum kwa kiwango kikubwa.

Amnesty Internatinal inataka uchunguzi ufanyike na Umoja wa Mataifa. Ombi ambalo serikali ya Ethiopia ilifutilia mbali mwezi Desemba.