KENYA- DIPLOMASIA

Joe Biden afanya mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuhusu masuala ya kikanda

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano wa umoja wa mataifa, desemba 3 2020.
Rais Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano wa umoja wa mataifa, desemba 3 2020. AP

Rais wa Marekani Joe Biden amempigia simu mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda, hasa kuhusu hali ya kiusalama na kibinadamu katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House, katika taarifa yake imesema kuwa viongozi hao wawili, Biden na Kenyatta, wamejadiliana kuhusu hali mbaya ya usalama na kibinadamu katika jimbo hilo, huku wakiafikiana kuwa kuna umuhimu wa kuzuia maafa zaidi na kuhakikisha kuwa msaada wa kibinadamu unawafikia watu walio katika eneo hilo.

Hata kabla ya mazungumzo kati ya Biden na Kenyatta, Marekani ilikuwa imeonesha wasiwasi wake kuhusu hali inayoendelea katika jimbo la Tigray, baada ya serikali ya Ethiopia kuanza mapambano na vikosi vya jimbo hilo mwezi novemba mwaka uliopita, na baadaye kutangaza ushindi.

Katika hatua nyingine, ripoti mpya ya shirika la Amnesty Intenational inaonesha kuwa wanajeshi wa Eritrea wametekeleza mauji ya watu katika jimbo hilo.

Afisa wa Amnesty International  Deprose Muchena amesema kilichotelezwa na wanajeshi hao na wale wa Ethiopia ni uhalifu wa kivita.

Ethiopia imekuwa ikikanusha kuwa iliwatumia wanajehsi wa Eritreea katika operehsni hiyo.