MALI - USALAMA

Wanajeshi 9 wameuawa nchini Mali

wanajeshi wa nchini Mali wakishika doria kwenye mji wa Gao.
wanajeshi wa nchini Mali wakishika doria kwenye mji wa Gao. AFP/Souleymane Ag Anara

Wanajeshi tisa wa Mali wamuawa katika mji wa Bandiagara, Uliopo eneo la kati la taifa la Mali, ambapo mji huo umekuwa ushuhudia mashambulizi ya mara kutoka kwa wanajihadi.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa idara ya jeshi ya Mali imesema tisa hao waliuawa alhamisi usiku.

Wanajeshi wangine tisa wanauguza majiraha mabaya kutokana na shambulizi hilo, wenyeji wakisema wanajeshi hao walikabiliana na wanajiahdi kwa muda mrefu.

Swala la usalama limesalia tata eneo la Sahel, ambapo wanajihadi wamekuwa wakifanya mashambulizi.

Kwa mjibu wa umoja wa mataifa, watu zaidi ya 4,000 wameuawa eneo la Sahel, kati ya mwaka 2016 hadi 2020, raia 770 wakidiriwa kuuawa mwaka 2016.

Wanajeshi wa Ufaransa 5,000 kwa ushirikiano na wale wa mataifa ya Sahel wanaenedelea kupamabana na wanajihadi hao.