Côte d’Ivoire yapokea chanjo ya kwanza dhidi ya COVID-19
Imechapishwa:
Côte d’Ivoire ni nchi ya pili katika bara la Afrika kupokea chanjo za bure dhidi ya Corona chini ya mpango wa Covax, ambao robo tatu inafadhiliwa na Ulaya na Marekani.
Dozi 500,000 za chanjo ya AstraZeneca ziliwasili jana Ijumaa na kupokelewa na mamlaka nchini Côte d’Ivoire, chanjo iliyotolewa kama sehemu ya mpango wa Covax.
"Chanjo zingine zitaletwa katika siku au wiki zijazo, kwa jumla ya dozi zaidi ya milioni mbili kama sehemu mpango huu wa Covax," ameahidi Jean-Marie Vianny Yaméogo, mwakilishi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Côte d’Ivoire.
"Côte d’Ivoire ni nchi ya pili ya Afrika kupokea chanjo hiyo lakini hasa ni nchi ya kwanza duniani ikwa kutoa chanjo kulingana na mpango wa Covax," amesifu Patrick Achi, katibu mkuu wa ikulu ya rais nchini Côte d’Ivoire.