CAMEROON-HAKI

HRW yalishtumu jeshi la Cameroon kwa mateso na mauaji dhidi ya raia

Askari wakipiga doria katika mji wa Bafut, kaskazini magharibi mwa Cameroon, katika eneo linalozungumza Kiingereza, Novemba 15, 2017 (picha ya kumbukumbu).
Askari wakipiga doria katika mji wa Bafut, kaskazini magharibi mwa Cameroon, katika eneo linalozungumza Kiingereza, Novemba 15, 2017 (picha ya kumbukumbu). AFP

Katika ripoti ya yake, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch (HRW) limewashutumu wanajeshi wa Cameroon kwa kutekeleza "mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi" kwa raia katika eneo linalozungumza Kiingereza katika miaka ya hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitekelezwa katika kijiji cha Ebam katika mkoa wa kusini magharibi mwa Cameroon ambapo wanawake wasiopungua 20 - ikiwa ni pamoja na wanne wenye ulemavu - walibakwa na wanaume karibu 30 walipigwa. Tukio hilo ulitokea mwaka mmoja uliopita, mnamo Machi 1, 2020, lakini dhulma hizo hazijawahi kuzungumzwa tangu wakati huo kwa hofu ya kufanyiwa vibaya au kuuawa kwa waathiriwa.

Kwa upande wa Ilaria Allegrozzi, mtafiti kwenye shirika la Human Rights Watch, anasema shambulio hilo ni ishara ya kile kinachotokea katika maeneo ya Cameroon yanayozungumza Kiingereza.

Shambulio huko Ebam sio jambo la kupuuzia. lilifanywa wiki mbili tu baada ya wanajeshi kuua raia 21 katika kijiji cha Ngarbuh, katika mkoa wa kaskazini magharibi.

Amnesty International imetaka mamlaka nchini Cameroon kufanya uchunguzi wa haraka kuhusu shambulio la Ebam.