UCHUNGUZI

Bunge la Seneti DRC lashtumiwa kutumia vibaya mali ya umma

Makao makuu ya Baraza la Bunge (DRC) wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge, Kinshasa, Septemba 15, 2016.
Makao makuu ya Baraza la Bunge (DRC) wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge, Kinshasa, Septemba 15, 2016. RFI/Sonia Rolley

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mamlaka ya ukaguzi wa Fedha nchini DRC (IGF) iko mbioni kukamilisha uchunguzi wake kuhusu matumizi ya fedha kwa mabunge mawili ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika Bunge la Seneti hasa, tangu kuingia madarakani kwa Felix Tshisekedi, kashfa zimeongezeka. Hasa, rais anayemaliza muda wake katika taasisi hiyo Alexis Thambwe Mwamba, rafiki wa karibu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila, anatajwa katika kashfa hizo.

Wakati Jumanne hii, Machi 2, 2021 kunatarajiwa kuchaguliwa na kuapishwa wajumbe wa ofisi mpya ya Bunge la Seneti, RFI imechunguza utumiaji wa fedha zilizotolewa kwa taasisi hii.

“Ofisi yoyote inayochunguzwa kwa kina inaweza kutupwa jela. Huu ndio ukweli kuhusu taasisi zetu. Kila kitu kinalipwa hapa, na pesa taslimu. Hakuna kitendo au kura ambayo kinachoweza kufanyika na maseneta au wabunge bila kulipwa kwa njia moja au nyingine ", amesema mmoja wa wabunge wa zamani nchini DRC.

Ingawa kwa muda mrefu kutoka muungano mmoja wa kisiasa, mbunge huyo amebaini kwamba yeye ni mfuasi wa Alexis Thambwe Mwamba au Eric Rubuye, rais wa ofisi ya bunge la Seneti linalomaliza muda wake na naibu wake.

Tangu mwezi Januari 2021, wawili hawa, washirika wa karibu wa rais wa zamani Joseph Kabila, wamekuwa wakilaumiwa vikali na Mamlaka ya ukaguzi wa Fedha nchini DRC (IGF) juu ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma. Wote wawili walijiuzulu, baada ya kuombwa kufanya hivyo na wajumbe wenzao wa taasisi hiyo kutokana na usimamizi mbaya. Hata hivyo Eric Rubuye yuko mafichoni. Aliondoka nchini baada ya kutoroka jaribio la kukamatwa.

"Sisemi wanapaswa kuadhibiwa kwa kile walichotenda, ninasisitiza tu kwamba uovu umezidi sana. Ikiwa hakungekuwa na mzozo kati ya rais Tshisekedi na mtangulizi wake, matukio ya mapema mwezi Januari, licha ya mgogoro wao kuonekana dhahiri, hayangejulikana, "seneta huyo wa zamani ameongeza.

Inaariwa kuwa zaidi ya dola Milioni tatu ziliondolewa kwenyeakanti ya benki ya Bunge la Seneti na kupelekwa nyumbani kwa rais wa taasisi hiyo. Tangu wakati huo kashfa kama hizo ziliendelea kuripotiwa katika Bunge la Seneti. Hali kama hiyo imekuwa ikiendelea.