AFRIKA KUSINI-AFYA-UCHUMI

COVID-19: Raia wa Afrka Kusini wakaribisha hatua ya rais Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Phill Magakoe / AFP

Afrika Kusini imechukua hatua ya kuanza kulegeza mashati ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kuanzia leo Jumatatu, baada ya visa vya maambukizi na vifo kupungua kwa kasi nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Jana Jumapili jioni katika hotuba yake kwa taifa, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza hatua mpya kulegeza vizuizi vilivyowekwa kwa kukabiliana na maambukizi ya janga la COVID-19 katika nchi hiyo iliyoathirika zaidi barani Afrika.

Hatua hiyo ambayo ilianza kutekelezwa Jumapili hii saa sita usiku, itawezesha kuanza tena kwa shughuli nyingi za kiuchumi nchini Afrika Kusini, ambazo zimeharibiwa sana na virusi vya Corona.

Katika hiotuba ya runinga, Cyril Ramaphosa aliripoti kupungua kwa kasi kwa visa vya maambukizi na wagonjwa hospitalini katika wiki nane zilizopita. "Kutokana na kupungua kwa idadi ya visa vya maambukizi, nchi sasa inaweza kulegeza vizuizi kadhaa kwenye shughuli za kusafiri na kiuchumi," alisema. "Tunafanya hivyo kwa uangalifu," aliongeza rais wa Afrika Kusini.

Kama matokeo, Afrika Kusini inahamia moja kwa moja kutoka kiwango cha 3 cha tahadhari hadi kiwango cha 1. Marufuku ya kutotoka nje nchini humo pia imefupishwa na sasa iitaanza kati ya usiku wa manane na saa 10 Alfajiri. Kulingana na rais Ramaphosa, Afrika Kusini imerekodi visa vipya visiozidi 10,000 vya maambukizi ya COVID-19 katika wiki iliyopita, ikilinganishwa na zaidi ya 40,000 katika wiki mwisho ya mwezi Januari na karibu 90 000 katika wiki ya mwisho ya mwezi Desemba 2020.