DRC-CENCO-SIASA-USALAMA

DRC: Cenco yatoa wito kwa rais Tshisekedi juu ya serikali ijayo

Wajumbe wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC.
Wajumbe wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC. REUTERS/Thomas Mukoya

Maaskofu Katoliki kutoka Baraza Kuu la Maaskofu nchini DRC (CENCO) bado wanakosoa utawala, hata baada ya urekebishaji wa mambo mbalimbali ya kisiasa unaoendelea na kuondolewa kwa washirika wa karibu wa Joseph Kabila katika uongozi wa taasisi za kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wao wa kwanza mwaka huu, Jumatatu wiki hii, Maaskofu Katoliki walikaribisha ujio wa viongozi wapya, ingawa mchakato wa kuwapata viongozi hao ukikumbwa na tuhuma za ufisadi kwa wabunge na maseneta na tuhuma za ukiukaji wa sheria za ndani za taasisi hizo za kisiasa nchini DRC.

Maaskofu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hali ya kisiasa nchini DRC, nchi yenye Wakristo wengi. Walikuwa wakilaani muungano kati ya Félix Tshisekedi (CASH) na Joseph Kabila (FCC) kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao. Mapema wiki hii, katika ujumbe wao uliowasilishwa na msemaji wao, Padri Donatien N’shole, CENCO iliendelea kuonyesha msimamo wake.

Padre Donatien Nshole, msemaji wa CENCO, Desemba 17, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Padre Donatien Nshole, msemaji wa CENCO, Desemba 17, 2019 (picha ya kumbukumbu). RFI/Pascal Mulegwa
Mabadiliko haya yalifanywa katika mazingira ya mvutano na kuibua maswali juu ya maadili ya vitendo hivi. Kujiunga katika Muungano Mtakatifu wa kitaifa haupaswi kuhamasishwa na msimamo wa kisiasa peke yake.

Waziri mpya akutana na wadau mbalimbali kuunda serikali mpya

Wakati Waziri Mkuu Jean - Michel Sama Lukonde akiendelea na mashauriano yake ya kuunda serikali ya kwanza baada ya Kabila, maaskofu wamesisitiza juu ya vigezo vya uteuzi na wamtka rais Tshisekedi kuwa makini.

"Wanaume na wanawake pekee ambao wameonyesha maadili mema katika siku zao za zamani na ambao wana uzoefu katika nafasi zinazohitajika, wanaojali ustawi wa raia, wanastahili kuteuliwa kusimamia taasisi za Serikali na mashirika ya umma. Watu watasikitishwa kuona wale walioshiriki katika uporaji, ukosefu wa usalama na ukiukaji wa haki za binadamu wakirudi madarakani. "

Katika serikali ijayo, wanomba "kufanya kila linalowezekana kushinda mvutano kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi wa kuaminika, wa wazi na amani mnamo mwaka 2023".

Maaskofu piawamegusia vurugu za makundi yenye silaha ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi Mashariki mwa nchi na kusema "wamesikitishwa sana na habari walizopokea na pengo kati ya ahadi zilizotolewa na ukweli juu ya kile kinachoendelea kwenye uwanja wa mambano".