DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Modeste Bahati Lukwebo, mgombea pekee wa urais wa Bunge la Seneti

DRC: Waziri wa zamani Modeste Bahati Lukwebo amemaliza kazi yake kuhafamisha na kubaini wabunge karibu 400 ambao ni sehemu ya muungano Mtakatifu (Januari 31, 2021).
DRC: Waziri wa zamani Modeste Bahati Lukwebo amemaliza kazi yake kuhafamisha na kubaini wabunge karibu 400 ambao ni sehemu ya muungano Mtakatifu (Januari 31, 2021). © Sonia Rolley / RFI

Uchaguzi wa wajumbe wa ofisi ya Bunge la Seneti utafanyika leo Jumanne, Machi 2. Pamoja na uchaguzi huu, rais Félix Tshisekedi ataungwa mkono na wajumbe kutoka mabunge yote mawili nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kufanikiwa kuwaweka washirika wake katika uongozi wa Baraza la Wawakilishi (Bunge), rais Félix Tshisekedi, ambaye alivunja muungano wake wa kisiasa na mtangulizi wake Joseph Kabila, hakupaswa hatakabiliwa na ugumu wowote katika kufanikisha azma yake, kutokana na upinzani ambao haupo kabisa katika Bunge la Seneti.

Ili kuongoza Bunge la Seneti, Félix Tshisekedi amemlenga Modeste Bahati Lukwebo. Yeye ndiye aliyefanya kazi ya kufahamisha kwa kutambua muungano mpya wa walio wengi bungeni, unaofaa kwa utawala wa sasa.

Mtu huyo anajua vema utaratibu unaotumiwa katika Baraza la Bunge nchini DRC. Mnamo mwezi Julai 2019, kwa wadhifa huo huo, alimuweka hatarini Alexis Thambwe, mgombea aliyeungwa mkono na rais wa zamani Joseph Kabila, na kupata kura 43 kati ya 108. Kwa kweli, Modeste Bahati Lukwebo alifaulu kuwashawishi maseneta wengine ambao walikuwa wafuasi wa muungano wa FCC wa Joseph Kabila wasifuate msimamo wa Joseph Kabila.

Leo amejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi. Muungano wa FCC umedhoofishwa. Wengi wamehama na, kulingana na rekodi za wanachama wa muungano Mtakatifu wa Jamhuri, maseneta 80 kati ya 108 wanamuunga mkono Félix Tshisekedi.