GUINEA-VYOMBO VYA HABARI-HAKI

Guinea: Mwanahabari Amadou Diouldé Diallo ashtakiwa kwa kumtukana rais

Magazeti ya Guinea kwenye soko la Madina huko Conakry (picha ya kumbukumbu).
Magazeti ya Guinea kwenye soko la Madina huko Conakry (picha ya kumbukumbu). Reuters / Emmanuel Braun

Mwandishi wa habari na mwanahistoria Amadou Diouldé Diallo anakabiliwa na mashitaka ya kumtukana rais wa Guinea Alpha Condé, madai ambayo yamefuliwa mbali na mwanasheria wake.

Matangazo ya kibiashara

Mwanahabari huyo yuko jela tangu jana usiku katika gereza la raia huko Conakry. Mawakili wake wanalaani kile wanachokiita "ukiukaji wa sheria ya uhuru wa vyombo vya habari," sheria ambayo inakataza mwandishi wa habari kufungwa kwa makosa ya kazi yake.

Amadou Diouldé Diallo alitekwa nyara Jumamosi na maafisa wa polisi kulingana na ndugu zake. Tangu wakati huo anashikiliwa katika majengo ya polisi na alijulishwa mashtaka yake Jumatatu jioni.

Shtaka ambalo mwanasheria wake, wakili Salifou Béavogui, akihojiwa na mwandishi wetu, Mouctar Bah, amefutilia mbali.

"Hatukutegemea kuwa anaweza kukamatwa kwa kudhalilisha kwa kiasi hiki! Sio tu mwandishi wa habari, lakini kosa la kumtukana mkuu wa nchi - ikiwa lipo - lilifanywa kupitia kazi yake ya uandishi wa habari, kwa sababu ilikuwa kwenye matangazo.

Mwendesha mashtaka wa umma ameamua kufungua uchunguzi wa kimahakama, kumshtaki mteja wetu kwa kosa lililotajwa kama "kumtukana rais wa nchi".

Mkuu wa majaji katika mahakama hiyo, aliomba mwandishi huyo wa habari awekwe kizuizini kwa muda, uamuzi ambao unapingwa na mwanasheria wake.