SUDAN KUSINI - AJALI

10 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini

Vibande vya mabaki ya ndege ilioanguka
Vibande vya mabaki ya ndege ilioanguka STR AFP

Watu 10 wakiwemo marubani wawili wamefariki nchini Sudan Kusini, baada ya ndege kuanguka jumanne jioni katika uwanja wa ndege wa Pieri, jimboni Jonglei.

Matangazo ya kibiashara

Akithibitisha ajali hiyo, gavana wa Jonglei, Denay Jock Chagor, amesema wamesitishwa na ajali hiyo ya ndege aina ya (HK-4274), ya shirika la South Sudan Supreme Airline, ambayo ilitokea jumanne mwendo wa 5.05 jioni.

Chagor amesema abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo pamoja na marubani wawili walifariki .

Uchuguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.