BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso : Sita waangamia baada ya gari waliokuwemo kukanyaga bomu Sahel

Wanajeshi wa Burkina Faso wakati wa mafunzo ya kijeshi Aprili,13,  2018 (picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa Burkina Faso wakati wa mafunzo ya kijeshi Aprili,13, 2018 (picha ya kumbukumbu). ISSOUF SANOGO / AFP

Watu sita, akiwemo mwanamke mja mzito na msichana mdogo wameuwa Kaskazini mwa Burkina Faso, baada ya gari la wagonjwa walilokuwa wanasafiria kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Ousseni Tamboura amesema gari hilo la wagonjwa lilikanyaga bomu hilo kati ya Gaskinde  na  Namissiguia katika jimbo la Sahel.

Watu hao waliouawa walikuwa wanaelekea katika mji mkuu Ouagadougou.

Mwezi Februari, wanawake wawili waliuawa baada ya mkokoteni waliyokuwa wanasafiria kukanyaga bomu katika mkoa wa Yagha Kaskazini mwa nchi hiyo.

Burkina Faso kama ilivyo kwa jirani zake Mali na Niger, zimeendelea kushuhudia mashambulizi kama haya hasa katika maeneo ya Kaskazini na Mashariki mwa nchi zao.

 Tangu kuanza kwa mashambulizi kama haya yanayotekelezwa na makundi ya kijihadi, mwaka 2015, watu zaidi ya 1,200 wamepoteza maisha na karibu Laki tano wameyakimbia makwao.