CHA-SIASA-USALAMA

Chad: Deby kuwania muhula wa sita

Rais wa Chad Idriss Deby.
Rais wa Chad Idriss Deby. POOL/AFP

Mahakama ya Juu nchini Chad, imesema rais Idris Deby, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, anaweza tena kuwania urais kwa muhula wa sita, wakati wananchi wa taifa hilo watakapopiga kura tarehe 11 mwezi Aprili.

Matangazo ya kibiashara

Sasa, Deby atamenyana na wagombea wengine tisa lakjini mpinzani wake mkuu Saleh Kebzabo, amejioondoa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya jaribio la kujaribu kumkamata mgombea mwingine wa upinzani Yaya Dillo.

Chad inaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa kati ya upinzani na chama tawala kuhusu hatua ya chama cha rais Idriss Deby kumteua rais huyo kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais kwa muhula wa sita.

Upinzani na baadhi ya mashirika ya wanaharakati wa haki za binadamu nchini Chad wamekuwa wakifanya kupinga hatua ya rais Idriss Deby Itno kuwania kwa muhula wa sita katika uchaguzi wa urais ujao.