Human Rights Watch yawashtumu wanajeshi wa Eritrea kuwauwa raia jimboni Tigray

Mwenyeji wa jimbo la Tigray akiomboleza kuuawa kwa wakaazi wenzake,  26 Februari 2021.
Mwenyeji wa jimbo la Tigray akiomboleza kuuawa kwa wakaazi wenzake, 26 Februari 2021. © AFP - Eduardo Soterase

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema wanajeshi wa Eritrea waliwauwa mamia ya watu wakiwemo watoto katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia mwezi Novemba mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii imekuja; baada ya Tume ya haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, kutoa ripoti kama hii na kuwashtumu wanajeshi wa Eritrea kutekeleza mauaji ya raia katika jimbo hilo hasa katika mji wa Axum.

Aidha, ripoti hii imetolewq wakati huu Jumuiya ya Kimataifa ikiendelea kulaani mauaji yaliyotokea katika jimbo hilo na kutaka uchunguzi huru kufanyika.

 

Wakuu wa Umoja wa Mataifa wanasema kilichotokea katika jimbo la Tigray ni uhalifu dhidi ya binadamu.

Hata hivyo, uongozi jijini Addis Ababa na Asmara umeendelea kukanusha kuwa vikosi vyake vilihusika na mauaji hayo.