SENEGAL

Senegal kukumbwa na maandamano mapya Jumatatu

Waandamanaji wakijikuta uso kwa uso n amaafisa wa usalama katika kata ya Colobane, Machi 5, 2021 Dakar, Senegal.
Waandamanaji wakijikuta uso kwa uso n amaafisa wa usalama katika kata ya Colobane, Machi 5, 2021 Dakar, Senegal. © AFP - SEYLLOU

Senegal inaendelea kukumbwa na maandamano ya upinzani na kesho Jumatatu kunatarajiwa kufanyika maandamo mapya makubwa, vuguvugu lililoundwa baada ya kukamatwa kwa mpinzani mkuu dhidi ya utawala umetoa wito wa maandamano mapya.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku tatu za machafuko mabaya zaidi kwa miaka kadhaa, nchi hiyo ambayo inachukuliwa kama kisiwa cha utulivu huko Afrika Magharibi kilipata utulivu iku ya Jumamosi. Walakini, vitendo vya uporaji vimeendelea kuripotiwa.

Kwa sababu mvutano huo haujakwisha. Vuguvugu la M2D, linalojumuisha chama cha mpinzani aliyekamatwa, vyama vya upinzani na vyama vya kiraia wametoa wito "kumiminika mitaani" kuanzia Jumatatu.

Hayo yanajiri wakati Ousmane Sonko, ambaye anazuiliwa kwa shutma za kutaka kuhatarisha usalama atafikishwa mahakamani Jumatatu Machi 8. Uamuzi wa majaji wa kumwachilia au kuendelea kumzuia unaweza kuchochea machafuko zaidi.