COTE D'IVOIRE

Mvutano waongezeka kati ya vyama vya siasa Côte d’Ivoire

Maafisa wa Tume ya uchaguzi (CEI) katika zoezi la kuhesabu kura baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura huko Abidjan Machi 6, 2021.
Maafisa wa Tume ya uchaguzi (CEI) katika zoezi la kuhesabu kura baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura huko Abidjan Machi 6, 2021. AFP - ISSOUF SANOGO

Chama tawala nchini Cote d’Ivoire cha RHDP kimepata ushindi katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumamosi ya wiki hii iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya Tume ya Uchaguzi yameonesha kuwa chama hicho cha rais Allasane Ouattara kimepata ushindi wa viti 147 kati ya 255 katika bunge hilo.

Hata hivyo, muungano wa vyama va upinzani vya marais wa zamani, Henri Konan Bedie na Laurent Gbagbo, vilivyoungana kwenye uchaguzi huu, navyo vimedai ushindi.

Kuibuka kwa mvutano kati ya kambi hizi mbili kubwa za kisiasa wasiwasi mkubwa waangalizi ambao wamezitaka pande hizo kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi na sio kuzua fujo na kutoa taarifa za mapema.