Senegal - Siasa

Senegal: Ousmane Sonko ashtakiwa lakini aachiliwa

Mwanasiasa wa upinzani Senegal, Ousmane Sonko.
Mwanasiasa wa upinzani Senegal, Ousmane Sonko. SEYLLOU / AFP

Mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, anayeshutumiwa makosa ya ubakaji, ameshtakiwa leo Jumatatu lakini ameachiliwa na kuwekwa chini ya usimamizi udhibiti wa mahakama baada ya kufikishwa mbele ya jaji, wakili wake ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kuachiliwa kwake kunaweza kusaidia kutuliza hali nchini Senegal baada ya ghasia za siku kadhaa zilizosababishwa na wafuasi wake, ambao wamepanga kuendelea na maandamano wiki hii.

Ousmane Sonko, mpinzani wa Rais Macky Sall, anafutlia mbali mashtaka dhidi yake ambayo anayachukulia kuwa yanachochewa kisiasa.

Watu kadhaa wanashikiliwa jela baada ya kukamatwa na vikosi vya usalama katika maandamano wakipinga kukamatwa kwa kiongozi wao.