EQUATORIAL GUINEA

Zaidi ya ishirini waangamia katika milipuko Equatorial Guinea

Milipuko iliyotokea katika ghala la silaha katika kambi ya jeshi katika mji mkuu za uchumi Equatorial Guinea imeharibu mali na vitu vingi.
Milipuko iliyotokea katika ghala la silaha katika kambi ya jeshi katika mji mkuu za uchumi Equatorial Guinea imeharibu mali na vitu vingi. © Reuters TV

Watu zaidi ya 2O wamefariki katika milipuko mikubwa iliotokea katika kambi ya jeshi katika mji wa Bata, mji mkuu wa uchumi wa Equatorial Guinea.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 600 walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea katika ghala la silaha, kulingana na ripoti rasmi ya awali.

Milipuko hiyo imesababishwa na "uzembe" uliohusishwa na hifadhi ya baruti kali kambini, rais wa Eguatorial Guinea amesema.

Rais Teodoro Obiang Nguema amesema katika taarifa kwamba athari iliyotokana na mlipuko huo "imesababisha uharibifu mkubwa wa mali na vitu huko Bata", na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia.

Katika mtandao wa Twitter, balozi wa Ufaransa Olivier Brochenin ametuma risala zake za rambi rambi kwa waathirika, akizungumzia ajali hiyo kama "janga".

Waziri wa afya wa Equatorial Guinea ameomba wahudumu wa afya kujitolea na kwenda katika hospitali ya eneo la Bata. Pia imetoa wito watu kujitolea kutoa damu kwasababu ya idadi kubwa ya waliojeruhiwa.