DRC - Usalama

Mkuu wa MONUSCO akutana na uongozi wa jimbo la Kivu Kaskazini

Kambi ya Monusco katika kata ya Boikene mjini Béni  Novemba 16 2018. (picha ya maonyesho)
Kambi ya Monusco katika kata ya Boikene mjini Béni Novemba 16 2018. (picha ya maonyesho) EUTERS/Samuel Mambo

Mkuu mpya wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo MONUSCO, Bintou Keita, siku ya jumanne amefanya ziara yake ya kwanza katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Alikutana na  gavana wa jimbo hilo  huo Carly Nzanzu Kasivita, mkuu mpya wa Monusco Bi. Bintou Keita amesema amani na utulivu katika eneo hilo la mashariki mwa nchi hiyo  ndio kipaumbele chake cha msingi kwa Tume ya Umoja wa mataifa.

Aidha, Mjumbe huyo Maalum wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  raia wa Guinea pamoja na Gavana Kasivita wamejadiliana kuhusu namna ya kuimarisha Usalama wa eneo hilo linalokumbwa na machafuko ya mara kwa mara, mauaji ya raia wasiokuwa na hatia kwenye miji na vijiji Kadhaa, ikiwemo wauaji yanayotekelezwa na waasi wa ADF wilayani Benin a viunga vyake, utekaji nyara huko Ruthsuru, na visa vya ukiukwaji wa Haki za binadamu.

 

Monusco ina wajibu wa kuisaidia serikali ya DRC katika kufanikisha miradi yake ya maendeleo hali kadhalika mbinu zake ili kuimarisha mamlaka ya serikali katika jimbo hilo lenye makundi mengi ya waasi.

Mbali na Goma, mkuu huyo wa Monusco pia atatembelea miji ya Bukavu huko Kivu kusini, pia Beni na Bunia jimboni Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.