Senegal - Siasa

Upinzani nchini Senegal waitisha maombolezo ya kitaifa na maandamano mapya

Maandamano ya upinzani yaliyofanyika nchini Senegal tarehe 8 Machi 2021, kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko.
Maandamano ya upinzani yaliyofanyika nchini Senegal tarehe 8 Machi 2021, kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko. AFP - JOHN WESSELS

Vuguvugu la upinzani nchini Senegal umeitsiha maandamano ya amani siku ya Jumamosi, kwa kile inachosema ni kuendelea kushinikiza uongozi wa rais Macky Sall kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, vuguvugu hili limeitisha maomboleo ya kitaufa siku ya Ijumaa, kuwakumbuka waandamanaji watano waliopoteza maisha, lakini upinzani unadai kuwa, waliopoteza maisha ni 11.

Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki ya pili sasa, kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani Ousamane Sonko aliyefunguliwa mashtaka ya ubakaji na kuchochea fujo.

Siku ya Jumatatu, Sonko, baada ya kushtakiwa aliachiliwa kwa dhamana huku akitoa wito wa maandamano ya amani.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa kuachiliwa kwake kunaweza kusaidia kutuliza hali nchini Senegal baada ya ghasia za siku kadhaa zilizosababishwa na wafuasi wake, ambao wamepanga kuendelea na maandamano wiki hii.

Ousmane Sonko, mpinzani wa Rais Macky Sall, anafutlia mbali mashtaka dhidi yake ambayo anayachukulia kuwa yanachochewa kisiasa, huku rais Sall akitoa wito wa utulivu.

Watu kadhaa wanashikiliwa jela baada ya kukamatwa na vikosi vya usalama katika maandamano wakipinga kukamatwa kwa kiongozi wao.