Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Hamed Bakayoko afariki dunia
Imechapishwa:
Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Hamed Bakayoko amefariki dunia akipatiwa matibabu nchini Ujerumani baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu.
Taarifa ya kifo cha waziri Mkuu huyo, ilitolewa kupitia runinga inayomilikiwa na serikali jijini Abidjan, baada ya rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kuichapisha kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akimtaja Bakayoko kuwa mfano mzuri kwa vijana wa nchi hiyo, mtu mwenye tabia ya aina yake mkarimu na mwaminifu.
Notre pays est en deuil.
— Alassane Ouattara (@AOuattara_PRCI) March 10, 2021
J’ai l’immense douleur de vous annoncer le décès du Premier Ministre, Hamed Bakayoko, Chef du Gouvernement, Ministre de La Défense, ce mercredi 10 mars 2021, en Allemagne, des suites d’un cancer. pic.twitter.com/IfImVNdlho
Bakayoko aliteuliwa katika nafasi hiyo miezi michache tu baada ya aliyekuwa waziri mkuu Amadou Coulibaly kuaga dunia, mwezi julai mwaka 2020.
Kifo chake kinakuja katika siku ambayo chama tawala cha RHDP ambacho ni chama chake kupata idadi kubwa ya viti katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika wiki iliyopita.
Rais Ouattara anatarajiwa kutoa tamko hivi leo katika kumuenzi mwanasiasa huyo ambaye zamani alikuwa mwandishi wa Habari, kiisha meya wa mji wa Abobo na mkufunzi wa vijana katika masuala mengi ya kijamii.
Hamed Bakayoko ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 56.