MAREKANI-ETHIOPIA

Biden asema anafuatilia kwa makini matukio katika jimbo la Tigray

Mzinga wa Jeshi la Ethiopia katika jimbo la Tigray
Mzinga wa Jeshi la Ethiopia katika jimbo la Tigray EDUARDO SOTERAS AFP/File

Rais wa Marekani Joe Biden anaguswa sana na mzozo unaoendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Jen Psaki, amesema Biden anafuatilia karibu ripoti za uhalifu wa binadamu kama mauaji ya raia na ubakaji wa wanawake na wasichana.

Aidha, amesema kuwa rais Biden anafahamu kuhusu hali mbaya ya kibinadamu na serikali yake inaendelea kutafuta mbinu za kuhakikisha kuzawa raia wanapata msaada na mashirika ya misaada yanapata nafasi ya kwenda katika jimbo hilo.

Mwezi Novemba mwaka 2020 jeshi la Ethiopia, lilianzisha operesheni dhidi ya vikosi vya TPLF katika jimbo hilo na imekuwa ikiripotiwa kuwa vikosi vya nchi hiyo na vile vya Eritrea, vimewauwa maelfu ya watu.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Mamboa ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema watu wa jimbo la Tigray wameendelea kushuhudia mauaji ya kikabila.

Ethiopia na Eritrea, zimeendelea kukanusha kuhusika na mauaji katika jimbo hilo.