DRC

Bunge la DRC kuanza rasmi vikao vyake

Katikati mwa mji mkuu wa DRC, Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu)
Katikati mwa mji mkuu wa DRC, Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu) Wikimedia/CC

Shughuli za Bunge zinaanza tena Jumatatu hii, Machi 15. Kikao cha kawaida cha Machi kinasubiriwa kwa hamu nchini DRC.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kinakuja baada ya mabadiliko ya kisiasa na kupinduliwa kwa walio wengi. Sasa ni Muungano mtakatifu kwa taifa ambao unachukua nafasi ya muungano wa FCC / CACH.

Kikao hiki cha kwanza kitatawaliwa hasa na uteuzi wa serikali ya Muungano mtakatifu kwa taifa, timu ya Waziri Mkuu Sama Lukonde. Moja ya mambo muhimu kwenye ajenda ya kikao hiki cha kawaida ni kuoneshwa na kuapishwa kwa wajumbe wa serikali hiyo mpya.

Waziri Mkuu aliyeteuliwa alilazimika kushauriana na wadau mbalimbali nchini DRC, wahusika katika masuala ya siasa, wajumbe kutoka vyama vya kiraia naviongozi mbalmbali ambao zaliungana na mpango wa rais Félix Antoine Tshisekedi.

Hoja zingine zitajadiliwa, ikiwa ni pamoja na kusasishwa kwa Tume Huru ya kitaifa ya Uchaguzi. Suala hilo limekuwa likijadiliwa Bungeni tangu mwezi Oktoba. Wengi wanajiuliza atakayechukua nafasi ya Corneille Nangaa katika uongozi wa Tume huru ya uchaguzi, CENI. Vyama mbalimbali vya kiraia havijaweza kukubaliana jina la mtu ambaye anaweza kuchukuwa nafasi hiyo. Suala ambalo linaweza kuzua mvutano mkubwa.