GAMBIA

Gambia: Hali ya utulivu yaanza kurejea Sanyang

Picha inayoonyesha vikosi vya usalama vya Gambia viliotumwa Banjul, Desemba 5, 2016 (picha ya kumbukumbu)
Picha inayoonyesha vikosi vya usalama vya Gambia viliotumwa Banjul, Desemba 5, 2016 (picha ya kumbukumbu) AP - Jerome Delay

Zaidi ya raia 250 wa Senegal, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Gambia, walitoroka kijiji cha uvuvi cha Sanyang, kilomita 40 kusini mwa Banjul, baada ya mapigano kati ya raia kutoka Senegal na raia wa Gambia wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Yote yalianza na kifo cha raia mmoja wa Gambia, aliyechomwa kisu usiku wa Machi 14 kuamkia Machi 15 ambaye alitendewa kitendo hiki na mvuvi kutoka Senegal ambaye alijaribu kumuibia. Ghasia zilizuka katika eneo hilo. Mamlaka nchini Senegal inajaribu kupunguza mivutano.

Mtu mmoja alipoteza maisha, biashara ziliibiwa, boti na kituo cha polisi vilichochomwa moto, familia za watu kadhaa kutoka Senegal zilikimbilia katika shule katika mji jirani wa Batokunku, chini ya ulinzi wa polisi wa Gambia… Walifikaje hapo? Bassirou Sène, balozi wa Senegal huko Banjul, amehoji:

Kwa mara ya kwanza, tumefikia kiwango hiki cha vurugu. Kulikuwa na jaribio la wizi, lililositishwa baada ya mtu mmoja kuchomwa kisu, na kujeruhiwa vibaya. Hivyo ndivyo ilivyoanza. Hatukutarajia hilo. Jamii ya watu kutoka Senegal inaishi kwa maelewano kamili na raia wa Gambia. Katika mji huo wa Sanyang, baadhi wameishi huko kwa kipindi cha miaka 50!