Kenya - Wakimbizi

Kambi za wakimbizi Kakuma na Dadaab kufungwa nchini Kenya

wakimbizi wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya  Kakuma nchini Kenya.
wakimbizi wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. AFP

Serikali ya Kenya, Kupitia kwa waziri wake wa usalama wa ndani, Fred Matiang'i imetoa makataa ya siku 14 kwa  kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab kufungwa, waziri  Matiang'i akisema hili limechangiwa na wimbi la tatu la virusi vya corona, serikali ikihofia kuwa huenda hali ikawa mbaya iwapo maambukizi ya corona itaripotiwa katika kambi hizo. serikali imeshutumiwa vikali na masharika ya kiraia  tume ya kutetea haki za kidamu ya KHRC, ikisema hatua hiyo ya serikali ni hatari zaidi kwa wakimbizi, Robert Waweru ni afisi wa mipango na uraia wa KHRC, nchini Kenya, alizungumza na Benson Wakoli.