DRC

Kesi ya Chebeya-Bazana DRC: Jenerali John Numbi akabiliwa na mashitaka

Picha ikimuonesha mkuu wa zamani wa Polisi nchini DRC, John Numbi  wa pili kulia ambaye anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Floribert Chebeya.
Picha ikimuonesha mkuu wa zamani wa Polisi nchini DRC, John Numbi wa pili kulia ambaye anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Floribert Chebeya. JUNIOR KANNAH / AFP

Mkuu wa zamani wa polisi nchini DRC John  Numbi ambaye anasakwa na mahakama ili kueleza kuhusika kwake katika kesi ya Chebeya, anaelezwa kuwa ameitoroka nchi hiyo na kukimbilia mafichoni wakati analengwa na waranti wa kukamatwa.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini DRC yanaomba serikali ya nchi hiyo kufanya kilio chini ya uwezo wake, afisa huyo wa ngazi ya juu katika polisi arejeshwe nchini.

Alitarajiwa kusikilizwa na mahakama ya kijeshi Alhamisi Machi 17 kuelezea kuhusika kwake katika mauaji  ya wanaharakati wawili wa haki za binadamu, Floribert Chebeya na dereva wake Fidèle Bazana, Juni 1, 2010. Lakini Jenerali John Numbi alipuuza wito huo kutoka ofisi ya mashtaka ya kijeshi: hakufanya safari kwenda Kinshasa.

Jumamosi Machi 20, maafisa wa idara ya ujasusi katika kijeshi walikwenda katika eneo linalojulikana kwa jina la Beijing, shamba la lake afisa huyo ambapo kawaida huishi wakati akiwa ziarani mjini Lubumbashi. Hata hivyo Mkuu wa zamani wa polisi hakuwapo.

John Numbi akimbilia mafichoni

Ofisi ya rais, pamoja na vyanzo vya jeshi huko Kinshasa, vinathibitisha kwamba waranti wa kukamatwa umetolewa dhidi ya jenerali huyo mtoro mwenye nyota nne. Kulingana na vyanzo hivyo, amepewa hifadhi ya ukimbizi katika nchi moja ya nchi za ukanda huo.

Hivi karibuni John Numbi alitajwa kama mdhamini wa mauaji ya Chebeya na Bazana na maafisa wawili wa polisi ambao wanadai kushiriki katika uhalifu huo: Kanali Christian Ngoy Kenga Kenga na Jacques Mugabo - wote wakiwa watoro kutoka kikosi cha Simba, pia walihusishwa, na ambao walikamatwa hapo awali huko Lubumbashi.

Vyama vya kiraia vimepaza sauti na kulaani uzembe au ulaji njama ambao umesababisha mkuu huyo wa zamani wa polisi kukwepa mahakama.