TOGO

Togo kuchukua hatua mpya dhidi ya COVID-19

Lomé, mji mkuu wa Togo.
Lomé, mji mkuu wa Togo. Creative commons Flickr CC BY-NC 2.0 Joshua Turner/Climate Centr

Togo imevuka kizingiti cha vifo vya watu 100 kutokana na janga la COVID-19 tangu mwishoni mwa juma hili lililopita, huku idadi ya visa vya maambukizi ikiendelea kuongezeka

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na kuzuka kwa aina mpya ya kirusi kilichoanzia Uingereza, visa vya maambukizi vinaongezeka na janga hilo linaendelea kusambaa haraka zaidi. Kutokana na hali hii, mamlaka inatarajia kuchukua hatua mpya katika siku chache zijazo.

Hali hiyo inachukuliwa kwa uangalifu mkubwa nchini Togo. Baraza la wataalam wa Sayansi na Rais wa Jamhuri, Faure Gnassingbé, wanaendelea kushauriana.

Janga la COVID-19 linasambaa haraka na visa vya maambukizi vimekuwa vingi. Mnamo mwezi Machi pekee, zaidi ya visa 2017 vya maambukizi na vifo 19 vilirekodiwa, ikilinganishwa na zaidi ya 18% ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Togo.

Hali hii ya wasiwasi inatokana na "sababu kadhaa" kulingana na Profesa Didier Koumavi Ekuévi, mwenyekiti wa Baraza la wataalam wa Sayansi: "Sababu ya kwanza ni kupungua kwa matumizi ya hatua za kudhbiti COVID-19. Sababu ya pili ni kusambaa kwa aina mpya ya kirusi kilichoanzia Uingereza, ambacho kimethibitishwa tu hivi karibuni, na kinasambaa haraka na kuua mara moja. Kuna pia kupuuziwa kwa ugonjwa huu, watu wenye dalili zinazoonyesha kuambukizwa virusi vya COVID-19 kupuuzia kufanya vipimo. "

Hali yatia wasiwasi lakini yaweza kudhibitiwa

Togo ilivuka kizingiti cha vifo vya watu 100 imwishoni mwa juma lililopita (vifo 104 kufikia Machi 23). Janga hilo limejikita karibu na mji mkuu Lomé, ameomgeza mwenyekiti wa Baraza la wataalam wa Sayansi. "Hali hiyo inatia wasiwasi lakini inaweza kudhibitiwa," alisema.

Kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 ilianza kwa chanjo ya AstraZeneca. Zaidi ya 92% ya wahudumu wa afya wamepewa chanjo hiyo. Kampeni hiyo itaendelea kwa wiki chache zijazo. Dozi mpya 45,000 za AstraZeneca tayari zimepokelewa, na hatua mpya za vizuizi zinatarajiwa kuchukuliwa katika siku zijazo ili kudhibiti maambukizi zaidi.